Madhumuni makuu ya MALENGO SACCOS LTD ni kuinua, kustawisha na kuboresha hali ya maisha ya wanachama ili waweze kukidhi mahitaji mbalimbali ya kijamii na kiuchumi kwa kufuata Masharti ya Chama, misingi na Sheria ya Vyama vya Ushirika
Neno toka kwa mwenyekiti
Ni ukweli ulio wazi kwamba, maisha ya mtanzania kujikwamua kiuchumi bado ni finyu. Ili watanzania wajikwamue sharti wajiunge kwenye umoja wao wa kuweka na kukopeshana na kuwekeza katika mashirika mabalimbali. Malengo saccos ni saccos bora yenye malengo makubwa katika kuleta mafanikio kwa wanachama na jamii nzima kwa ujumla. Ni nafasi pekee ya sisi kuungana katika safari yetu ya mafanikio, malengo yetu mafanikio yetu.